SURA KAMILI YA MWEZI WA TOBA

ztcc gathering
SURA KAMILI YA MWEZI WA TOBA

Mwezi wa toba ndio mwezi wa kwanza wa mwaka wa kukumbatiwa na Mungu. Ndio hatua yetu ya kwanza baada ya kuvuka kutoka mwaka wa 2023 kuelekea mwaka 2024. Kama hatua ya kwanza ya kuingia katika uzuri wa Mungu hakika kwa watu wake, tukiingiya tukiwa na mioyo mikunjufu pia yenye kutubu.

Mwezi wa januari umekuwa pia mwezi wa mageuzi kwa wanamemba wote wa ki otantike duniani pote. Ulikuwa ni mda wa kuamua, mda wa mageuzi na mda kukomaa kiroho katika safari yetu na Mungu. Lakini pia hii ilikuwa ni mwanzo wa safari yetu, kwa sababu njia ya kuingia na kukaa kwenye ahadi zetu na Mungu inaendelea.

NI YAPI YALIYO TOKEYA KATIKA MWEZI HUU WA TOBA?

Kila wiki, kila siku na saa baada ya nyingine ni vya muhimu mbele ya macho ya Bwana, kama jibukwa waamini na wateule washirika la kiotantike pamoja na washirika wote wa zion temple, kila wiki na kila siku ilikuwa na tafsiri yake katika mda huu wa kutubu ili kuingia kwa wakati wa uamsho na kwa kila jambo la maisha na tumebarikiwa pia kuungana na mzazi wetu kwa mwezi huu wote.

WIKI YA MWITO WA TOBA

Kutubu siyo mda wa kuyarudilia makosa ya binadamu pia si mda wa kutoa madhabahu ya damu ili kutuliza hasira ya mungu, bali ni kukubali na kutarajia kwa roho za binadamu kumugeukia Mungu. Kama vile tunavyo ishi na kuwa na historia tofauti, mambo mengi zaidi ya moja huumbika ndani ya roho zetu, lakini Mungu pekee ndiye mwenyewe anastahili kutongoza na kutawala kikamilifu mioyo yetu. Wiki hii imeandaliwa ili kujionja na kutafakari kwa ajili yako binafsi na kuita roho mtakatifu kutufunuliayale majaribu kwa mafikiri yetu na hata kwa yale yanayo tuzunguka ili tupate kumugeukia Mungu kikamilifu.

Haya si kwetu tu, bali pia kwa wanamemba wote na pia kwa inchi yetu. Kwa sababu watenda dhambi huongozwa na mwili na kupokeya pigo za muovu na pia hasira ya Mungu siku ya hukumu.

repantance

MAANDIKO MATAKATIFU

Yoeli 2:12-14: 12“Lakini sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia na kwa kuombolea”. 13Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, Mkamrudilie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndie mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa

rehema naye hughairi mabaya. 14Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia Baraka nyuma yake, naam sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana Mungu wenu?.

Ni mpango wa Mungu kuishi pamoja na watu wake, kuongea nao, kufanya kazi pamoja nona kutembea pamoja nao katika mwaka huu wa kukumbatiwa naye. Lakini Mungu hawezi kutumika na watu wenye roho mbili wala wenye mioyo yenye kuwa mbali na Mungu na wale ambao pia wameamua kutoa sadaka kubwa na isiyo ya kawaida. Hiyo ndio sababu anatukubali katika neema na fadhili zake, anatukubali kutubu kwa namna yoyote ya dunia naya kimwili na kuingia katika uzima wa mbinguni katika Yesu kristo!.

MWEZI WA UMOJA KATIKA MWILI WA KRISTO

Katika utaratibu wa nyakati hizi za toba, inatofautisha ya kwamba sasa mwili wa kristo utakuwa mmoja tena kwa umoja katika kristo Yesu. Adui wetu ni matengano, lakini Bwana wetu Yesu ni mpenzi wa umoja kwa sababu ni mmoja na baba pamoja na roho mtakatifu. Katika Biblia, kutoka katika agano la kale hadi agano jipya, tumepata nguvu kubwa zikizihirishwa wakati wawili ama zaidi ya wawili wakiungana kwa pamoja na kukubaliana. Kwa wakati huu wa uamsho, tunaombwa kuishika dunia na kugeuza njia zote za umoja wetu, tukiomba pia kunyenyekea, tukiabudu Bwana wetu. Acheni ufalme wa Mungu pekee. Tumeona pia kupitia mafundisho ya baba yetu Mtume Dr. Gitwaza Paul, kama ufalme wa giza hutumia mbinu hizi ili kuwapotosha watoto wa Mungu.

body of christ together

MAANDIKO MATAKATIFU

Yohana17:21:Wote wawe na umoja; kama we, baba, ulivyo ndani yangu, name ndani yako, ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

1 Wafalme 18:30-33: 30Kisha Eliya akawaambiya watu wote, nikaribieni mimi, watu wote wakamkaribia. Akatengeneza madhabahu ya Bwana iliyovunjika. 31Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo, aliyejiiliwa na neno la Bwana na kuambiwa, jina lako litakuwa Israeli. 32Naye akajenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana, akafanya mfereji kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu. 33Kishaakazipanga zile kuni, akamkata yule ng’ombe vipand vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni.

Mwito huu wa umoja umefwatiwa na wiki nzima ya kufunga na kuomba katika umoja. Tumeona kazi tofauti za mwovu kupitia nzige, tofauti zao na mapigo zao kwa waamini. Na kwa upande mwingine, tumeona nguvu na uwezo wa Yesu Kristo anaye onekana katika sura ya mkulaji wa nzige, na akisimama kupiganisha kazi zote za mwovu. Wiki imekomeshwa na kazi nzuri ya kuombea umoja wa wa inchi zetu, na kupokeya mipango ya Mungu kwa inchi za maziwa makuu, akili, uzuri na utajiri kwa inchi zetu.

WIKI YA KUCHAGUA UTAKAYE MUTUMIKIA: “Mungu ao Shetani”.

Nyuma ya wiki ya kufunga na kuomba, ni wakati sasa wa kujitoa kwa Bwana, mwili, moyo na roho zetu, ni wakati pia wa ku piga hatua zinazo onyesha muelekeo wetu. Mwanadamu ana uwezo wa kuamua, ingawa tujue wala tusijue na uamzi huo, tupende wala tusipende ndiyo inaonyesha muongozo na yale yanayo tufikia kwa maisha yetu. Tumebarikiwa kuongozwa na mzazi wetu Myume Dr. Paul Gitwaza, ambaye ana ujumbe kamili kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ametuonyesha namna gani ya kuchagua nani tumutumikiye, pamoja na mifano kutoka katika kitabu cha Biblia, ambapo wanawake na wanaume ambao wamechagua vizuri na kubadilisha maisha yao. Mfano wa Jemadari kama Yoshua amachagua kumtumikia Mungu na wengine kama mfalme Ahabu ambaye amechagua kuitumikia miungu ya wakanani nay ale yote yalio mufikia.

MAANDIKO MATAKATIFU

Yoshua 24:14-15: 14Basi sasa mcheni Bwana, mkamtumikie kwa unyofu, wa moyo na kwa kweli, na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya mto, na huko Misri, mkamtumikie yeye Bwana. 15Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakaye mtumikia, kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu walimtumikia ng’ambo yam to, ao kwamba ni miungu ya wale wamori ambao mnakaa katika inchi yao, Lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.

1 Wafalme 18:20-21: 20Basi, Ahabu akapeleka watu, kwa wana wa Israeli wote, akawakusanya manabii pamoja katika mlima wa karmeli. 21Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, mtasita sita katikati ya mawazo mawili hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu mfuatani, bali ikiwa Baali ni mungu, Haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.

1 wakorintho 10:18-22: 18Waangalieni hao wa Israeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili, wale wazilao dhabihu, je hawana shirika na madhabahu? 19Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilicho tolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Ao ya kwamba sanamu ni kitu? 20Sivyo, lakini vitu vile wavitowavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu, name sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.

21Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22

Au twamtia Bwana wivu? Je tuna nguvu zaidi ya yeye?

Uamzi si kitu rahisi, zaidi sana katika ulimwengu wa kiroho, na kwa Mungu hakuna njia mbili wala njia kadhaa, nikuwa pamoja nami wala haupo pamoja name. wiki hii ilikuwa ya kuchagua. Ni nani unayempa muda wako? Ni nani unamwamini? Kwa sababu uamzi wako leo, ndio utangoza matarjio yako.

Mzazi wetu ametufndisha ginsi uamzi wetu unanongozwa na ujuzi kutoka misri, ambo ni tafsiri na ujuzi wa mbinu za dunia ambazo zinaongozwa na miungu ya kanani, mazingira, historia zetu, familia na kadhalika. Ndizo sababu katika mwaka huu wa kukumbatiwa na Mungu, tumeitwa kujifunza neno la Mungu, kuomba na kuwa na uhusiano na roho mtakatifu ili kutakaswa na kuweza kuamua Mungu zidi ya vitu vyote.

WIKI YA TOBA ILETAYO FARAJA

Wiki hii ilikuwa wiki ya Baraka sana, tumeneemika kubarikiwa na mtumishi wa Mungu ambaye ametembeya na Mungu kwa mda mrefu, huyu si mwengine ni Mtume mama Domitille Nabibone. Wateule wa Mungu walikusanyika katika kanisa letu la Gatenga ili kusikiliza na kujifunza kupitia miiujiza kutoka mbinguni na yerusalemu mpya ambayo Mungu ameandalia walio wake.

Ushuhuda umewasaidia waumini wengi kufikiria mara tena kwa mwenendo wao, kuona ya kwamba yale walio kuwa wakiwaza kwamba hayawezekani duniani, wameelewa ya kwamba yanawezekana. Katika ushuhuda huo, mtumishi wa Mungu amechangia safari yake ya kuingia mbinguni, na matendo yetu yetu yana tafsiri na majibu kutoka mbinguni.

Ulikuwa pia mda wa kutubu na kuacha dhambi zote, tabia amabazo zinatuzuia kuingia mbinguni. Kukutana na Mungu kwa mtumishi wake inamaanisha ya kwamba inawezekana kutembeya na Mungu na kumtumikia Mungu katika nguvu lakini kwa hayo yote tunaombwa kuwa na unyenyekevu, utakaso na Roho yenye kumcha Mungu peke yake.

Katika myaka yake ya ukubwa, angali na moto wa kuitangaza injili, mabadiliko ya siku kwa siku ya Roho mtakatifu, kama ilivyo kwa kila muaminifu yeyote, tujivuwe mavazi ya dhambi kwa kutubu.

MAANDIKO MATAKATIFU

MatendoyaMitume3:19: Tubuni basi mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.

Mwanzo26:25:Akajenga madhabahu huko, akalitia jina la Bwana. Akapiga hema yake huko, na watumwa Isaka wakachimba kisima huko.

Mzazi wetu mtume Paul Gitwaza, ameyaongea hayo wakati tulipokuwa tukifundishwa nguvu zilizomo kwa kumtwika Yesu mizigo yetu, wakati tunapo asi roho mtakatifu hutuma upepo wa kutibu na kutugeuza kuwa wapya na kutusamehe makosa yetu yote na kutukaribisha kwa ufalme wa mbinguni.

Mungu hutuita ili kutubu na kuachana na dhambi. Msamaha mzuri ni kutubu na kugeuka, bila mageuzi hakuna msamaha kamili. Mungu hutaka sisi kuleta vyote vinavyo tulemelea msalabani na kufurahia ukombozi na neema tupatayo toka kwa Mungu.

MENGINE UNAYO YAHITAJI KUJUA

Katika mengi unayo hitaji kuyajua, kumeanzishwa chuo cha biashara ao uchumi (banki) TC KIRA, imefunguwa milango yake na inatumika vizuri. Ingekuwa heri kwa kila mwana memba yeyote wa Zion Temple na wengine kujiandikisha kama wana memba wa shirika hilo. Kwa sababu macho yetu yanatazama mbele kwa ajili ya maendeleo ya benki hiyo na pamoja na Yesu yote yawezekana.

Chuo hiki cha biashara kimetoka katika mawazo ya Mungu kwa watu wake, kwa sababu Mungu atahusika na mambo yetu, hii ni moja wapo kati ya mengi Mungu ameandaa kutubariki. Basi tungekuomba kutobaki nyuma kwa wakati huu, uwe mumoja katika wengi wabarikiwa, tunayo matawi yetu Nyabugogo, Remera Giporoso na kwenye kituo kikuu cya AWM Gatenga.

CHUO CHA MAENDELEO (ADA)

Chuo hicho kinahusika zaidi na vijana, hayo yatokana na mapenzi mazuri ya mzazi wetu ya kuwapa vijana kuingiya kwa ahadi ya Mungu. Ndiyo maana ADA imewatufuta washirika na kuanzisha mipango ya kuinua, kuwapa nguvu na kugeuza vijana kuwa wanzilishi wa mabadiliko katika ufalme wa Mungu na katika jamii waliomo. Katika mwezi wa januari, ADA pamoja na chuo ALX

kwa kutia Rafiki za Daniel, katika mpango wa teknologia ambao umeandaliwa kwa kibinafsi katika kazi zao na kwenye soko la biashara.

IBADA YA VIJANA PAMOJA NA MTUME Dr. GITWAZA PAUL

Hii ni mufululizo wa ushuhuda, mda wa maombi, mda wa neno la hekima kutoka kwa mzazi wetu. Haya yanaleta mabadiliko makali sana kwa vijana wote duniani na katika nchi ya Rwanda kama tulivyoshinda kupitia neno la ushuhuda. Huu ni mda wa kujifunza na kutubu pia vijana wengi wameokoka katika ibada hii Mtume amewaahidi kuendelea katika mwezi wa pili ambao ni mwei wa moto.

KARIBUNI SANA KWA MWEZI HUU WA “MOTO”.

Tumeingia katika mwezi wa pili ama wa februari, mwezi wa “MOTO” ni mwezi wa uamsho mkali. Katika mwezi wa “TOBA” ama mwezi wa januari, tumeona moto ukishuka kutoka mbinguni ili kuteketeza madhabahu, wakati wa nabii Eliya, ndiyo sababu tunatarajia kupata hatua zingine za moto, katika mwezi huu tutakuwa nawakati mwingine wa mafungo na maombi pia ibada za uamsho kila jioni pamoja na Mtume Dr. Paul Gitwaza. Tunasubir kwa hamu kuu kuona ginsi Mungu atahusika kwa ajili yako katika mwezi huu wote.

Mungu awabariki SHALOM!!!!